Viashiria vya kujiua: Uchunguzi wa mhusika kazimoto katika riwaya ya kichwamaji

Thumbnail Image

Date

2024

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Journal of Kiswahili and Other African Languages

Abstract

Wahusika katika kazi za fasihi huumbwa kwa ustadi mkubwa kwa lengo la kubeba tafakuri na fikra za mtunzi kuhusu maisha ya jamii. Katika uumbaji huo, aghalabu, binadamu husawiriwa kama kiumbe anayeteseka na anayeishi katika ulimwengu usiomjali, aliyezungukwa na mateso na ubwege1, na anayeshindwa kukabiliana vyema na uhalisia wake (Wamitila, 2002). Mambo hayo, ndiyo huweza kusababisha afanye maamuzi fulani kama vile kujiua. Hivi ndivyo anavyofanya Euphrase Kezilahabi katika riwaya ya Kichwamaji (1974) anapomuumba mhusika anayejiua.Hata hivyo, kwa kuwa kujiua huambatana na viashiria mbalimbali, makala haya yanajadili viashiria vya kujiua kwa mhusika mkuu katika riwaya teule tu. Riwaya hiyo imeteuliwa kwa sababu ina mawanda ya kutosha yaliyowezesha kupata data zilizolengwa katika makala haya. Pia, riwaya hiyo imeteuliwa kama sampuli ya kuwakilisha riwaya nyingine zenye viashiria vya kujiua. Misingi ya Nadharia ya Udhanaishi imetumika katika uchunguzi, uchanganuzi na uwasilishaji wa matokeo. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa matini. Mjadala umebainisha kwamba katika riwaya ya Kichwamaji vipo viashiria vinne vya kujiua vilivyomkumba Kazimoto kabla ya kujiua kwake. Viashiria hivyo ni kukata tamaa, kujitenga kijamii, kuzungumzia masuala ya kujiua na mabadiliko ya tabia. Makala yanahitimisha kwamba jamii inahitaji kupewa elimu ya kutosha kuhusu kujiua kwa wahusika pamoja na viashiria vyake ili iweze kumtambua na kumsaidia mtu mwenye viashiria vya kujiua.

Description

Paper submitted to the " Journal of Kiswahili and Other African Languages " for publication purposes

Keywords

Kujiua (Suicide) - Tanzania, bwege, Viashiria, Nadharia ya Udhanaishi, Euphrase Kezilahabi, Viashiria vya kujiua (Suicidal indicators), Kichwamaji, Mhusika Kazimoto, Riwaya ya Kiswahili, Saikolojia katika Fasihi, Fasihi ya Kiswahili — Uhakiki na Uchunguzi (Swahili literature — History and criticism), Kujiua katika Fasihi (Suicide in literature), Saikolojia na Fasihi (Psychology and literature), Maadili na Jamii katika Fasihi ya Kiswahili.

Citation

APA

Collections

Endorsement

Review

Supplemented By

Referenced By