Viashiria vya kujiua: Uchunguzi wa mhusika kazimoto katika riwaya ya kichwamaji

dc.contributor.authorFuluge, Adria
dc.date.accessioned2026-04-13T11:10:39Z
dc.date.issued2024
dc.descriptionPaper submitted to the " Journal of Kiswahili and Other African Languages " for publication purposes
dc.description.abstractWahusika katika kazi za fasihi huumbwa kwa ustadi mkubwa kwa lengo la kubeba tafakuri na fikra za mtunzi kuhusu maisha ya jamii. Katika uumbaji huo, aghalabu, binadamu husawiriwa kama kiumbe anayeteseka na anayeishi katika ulimwengu usiomjali, aliyezungukwa na mateso na ubwege1, na anayeshindwa kukabiliana vyema na uhalisia wake (Wamitila, 2002). Mambo hayo, ndiyo huweza kusababisha afanye maamuzi fulani kama vile kujiua. Hivi ndivyo anavyofanya Euphrase Kezilahabi katika riwaya ya Kichwamaji (1974) anapomuumba mhusika anayejiua.Hata hivyo, kwa kuwa kujiua huambatana na viashiria mbalimbali, makala haya yanajadili viashiria vya kujiua kwa mhusika mkuu katika riwaya teule tu. Riwaya hiyo imeteuliwa kwa sababu ina mawanda ya kutosha yaliyowezesha kupata data zilizolengwa katika makala haya. Pia, riwaya hiyo imeteuliwa kama sampuli ya kuwakilisha riwaya nyingine zenye viashiria vya kujiua. Misingi ya Nadharia ya Udhanaishi imetumika katika uchunguzi, uchanganuzi na uwasilishaji wa matokeo. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa matini. Mjadala umebainisha kwamba katika riwaya ya Kichwamaji vipo viashiria vinne vya kujiua vilivyomkumba Kazimoto kabla ya kujiua kwake. Viashiria hivyo ni kukata tamaa, kujitenga kijamii, kuzungumzia masuala ya kujiua na mabadiliko ya tabia. Makala yanahitimisha kwamba jamii inahitaji kupewa elimu ya kutosha kuhusu kujiua kwa wahusika pamoja na viashiria vyake ili iweze kumtambua na kumsaidia mtu mwenye viashiria vya kujiua.
dc.description.sponsorshipPrivate
dc.identifier.citationAPA
dc.identifier.issnOnline): 2958-4914
dc.identifier.urihttps://doi.org/10.58721/jkal.v2i1.548
dc.identifier.urihttps://scholar.mzumbe.ac.tz/handle/123456789/1950
dc.language.isoother
dc.publisherJournal of Kiswahili and Other African Languages
dc.subjectKujiua (Suicide) - Tanzania
dc.subjectbwege
dc.subjectViashiria
dc.subjectNadharia ya Udhanaishi
dc.subjectEuphrase Kezilahabi
dc.subjectViashiria vya kujiua (Suicidal indicators)
dc.subjectKichwamaji
dc.subjectMhusika Kazimoto
dc.subjectRiwaya ya Kiswahili
dc.subjectSaikolojia katika Fasihi
dc.subjectFasihi ya Kiswahili — Uhakiki na Uchunguzi (Swahili literature — History and criticism)
dc.subjectKujiua katika Fasihi (Suicide in literature)
dc.subjectSaikolojia na Fasihi (Psychology and literature)
dc.subjectMaadili na Jamii katika Fasihi ya Kiswahili.
dc.titleViashiria vya kujiua: Uchunguzi wa mhusika kazimoto katika riwaya ya kichwamaji
dc.typeArticle

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Thumbnail Image
Name:
Fuluge, A.- FSS.- (2024).pdf
Size:
288.59 KB
Format:
Adobe Portable Document Format

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed to upon submission
Description:

Collections