Research Papers
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Research Papers by Subject "Usawiri wa Eskatologia"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Usawiri wa eskatolojia ya Waafrika katika mbolezi za Wangoni(CHALUFAKITA 2020, JUZ. NA. 2, 2020) Duwe, MartinaEskatolojia ni kipengele kimojawapo kinachodhihirisha falsafa ya jamii za Waafrika kulingana na mila na desturi zao. Tafiti nyingi zilizofanywa kuhusu dhana hii zimejiegemeza katika muktadha wa kiteolojia. Baadhi ya tafiti hizo ni zile zilizofanywa na Baloyi (2008) na Lup (2013). Licha ya kuwapo kwa tafiti hizo, dhana ya eskatolojia ya Waafrika hususani fasihi simulizi za jamii ya Wangoni bado haijamakinikiwa ipasavyo. Aidha, ni wazi kwamba fasihi simulizi ni fasihi inayobeba na kuibua maarifa ya kifalsafa yanayoisawiri jamii husika kulingana na kaida zao. Kwa mantiki hiyo, makala hii inajadili usawiri wa eskatolojia ya Waafrika katika kipera cha mbolezi hususani za jamii ya Wangoni ili kubainisha maarifa yanayobebwa katika kipera hicho. Makala hii ni matokeo ya utafiti uliofanyika kwa kutumia mbinu ya ushuhudiaji shirikishi katika matukio yanayoambatana na suala la kifo na mahojiano ya ana kwa ana na baadhi ya Wangoni katika mazingira yao halisi. Data zimechanganuliwa kwa njia ya maelezo. Data hizo zinaonesha kuwapo kwa eskatolojia ya Waafrika katika mbolezi za jamii hiyo. Hata hivyo, makala hii inajadili vipengele muhimu vitatu tu ambavyo ni: kuamini katika uwepo wa Mungu, mwendelezo wa maisha baada ya kifo na nguvu za waliokufa (mizimu).