Majukumu ya msingi ya Maktaba katika kuleta mabadiliko kwenye sekta yaelimu nchini Tanzania: Uchunguzi yakinifu

No Thumbnail Available
Date
2022-11-24
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Tanzania Library Service Board (TLSB)
Abstract
Sekta ya elimu ni msingi wa maendeleo ya taifa, inatoa mchango na nguvu na ya kuboresha maisha ya watu. Elimu ni haki ya msingi kwa kila mtu. Maktaba na elimu ni dhana zisizotenganishwa; maktaba ni sehemu muhimu ya taasisi za elimu, zikichangia katika kujisomea na utafiti. Utafiti umebainisha kuwa maktaba ni muhimu katika kuimarisha hamu (reading passion) ya kusoma na kuongeza ujuzi wa wanafunzi. Mwongozo wa Viwango na Sheria ya Elimu ya Vyuo Vikuu Tanzania unaweka viwango vya maktaba kwa vyuo vikuu ili kuhakikisha ubora wa elimu. Katika miaka ya 1970, Tanzania ilianzisha maktaba za vijijini kusaidia Elimu ya Watu Wazima na kuongeza kiwango cha kusoma na kuandika. Hata hivyo, kiwango cha elimu kimeshuka tangu miaka ya 1990 kutokana na changamoto kama ukosefu wa wakutubi wenye ujuzi, bajeti pungufu, na ukosefu wa maktaba za kisasa. Ili kuboresha elimu, huduma ya maktaba shuleni inapaswa kupewa kipaumbele. Maktaba zinahitaji bajeti ya kutosha, vitabu vya kisasa, na teknolojia ya kidigitali. Pia, maktaba zishirikiane na wadau wengine na kutumia mitandao ya kijamii kuwafikia watumiaji hususani wanafunzi. Maktaba ni muhimu kwa kila mkakati wa kisomo, elimu, na maendeleo ya kijamii. Zinaweza kuwa sehemu ya uvumbuzi wa maarifa na kutoa huduma zinazolenga mahitaji ya watumiaji. Kuwa na maktaba bora kutasaidia kuboresha elimu na maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Description
Makala iliyowasilishwa katika Kongamano la Pili la Kitaifa kuhusu Kuboresha Utoaji wa Huduma za Maktaba na Habari nchini Tanzania, Kukuza Usomaji kwa Watoto na Maonyesho ya Vitabu yaliyofanyika kuanzia tarehe 23 hadi 24 Novemba 2022 katika Hoteli ya Tanga Beach Resort na SPA. Mada: Mchango wa Huduma za Maktaba, Utunzaji wa Nyaraka na Mafunzo ya Ukutubi katika Uboreshaji wa Elimu Tanzania.
Keywords
Elimu na Maktaba – Tanzania, Maktaba za Vijijini, Mpango wa Elimu ya Watu Wazima – Tanzania, Maktaba za Shule – Tanzania, Huduma ya Maktaba, Maktaba na Sekta ya Elimu, Maktaba na Mabadiliko ya Elimu – Tanzania, Maktaba za kidigiti
Citation
APA