Majuto ni mjukuu: Uchunguzi wa mhusika Ngoma katika riwaya ya ua la faraja

dc.contributor.authorFuluge, Adria
dc.date.accessioned2026-08-28T07:17:49Z
dc.date.issued2024
dc.descriptionPaper submitted for publication in the Journal of Linguistics, Literary and Communication Studies
dc.description.abstractMaisha ya mtu ni hadithi inayopaswa kusimuliwa ili kutoa mafunzo kwa jamii kuhusu mapito ya mhusika. Hii inatokana na ukweli kwamba kila mtu katika jamii ana mambo mazuri na/au mabaya ya kusimulia yanayohusu mapito ya maisha yake. Yapo masimulizi yanayofurahisha kutokana na matendo ya mhusika na mengine husikitisha kiasi cha kumfanya mhusika kuyajutia maisha yake kutokana na kufanya au kutofanya jambo fulani. Kwa msingi huo, makala hii ililenga kuchunguza methali inayosema “majuto ni mjukuu” kwa kuchunguza maisha ya mhusika Ngoma katika riwaya ya Ua la Faraja (2004). Mhusika huyu ameteuliwa kama kiwakilishi cha wahusika wengi ambao katika maisha yao, walifanya na/au hawakufanya mambo fulani ambapo kutokana na kufanya na/au kutokufanya kwao, kulisababisha majuto katika maisha yao. Pia, riwaya hii imeteuliwa kama sampuli ya riwaya mbalimbali zenye wahusika wenye sifa kama za mhusika Ngoma. Data zilitokana na uchambuzi wa riwaya ya Ua la Faraja. Vilevile, Nadharia ya Uhalisia ilitumika kama mwongozo katika ukusanyaji wa data, uchambuzi na uwasilishaji wa matokeo ya utafiti wa makala hii. Matokeo yanaonesha kwamba ziko sababu kuu nne zilizosababisha Ngoma ayajutie maisha yake. Sababu hizo ni kukosa uaminifu katika ndoa, kuitelekeza familia yake, kuendekeza anasa, na kutowajali ndugu zake.
dc.description.sponsorshipPrivate
dc.identifier.citationAPA
dc.identifier.urihttps://doi.org/10.58721/jkal.v2i2.863
dc.identifier.urihttps://scholar.mzumbe.ac.tz/handle/123456789/2204
dc.language.isoother
dc.publisherJournal of Linguistics, Literary and Communication Studies
dc.subjectMajuto
dc.subjectMethali
dc.subjectMhusika
dc.subjectMjukuu
dc.subjectCharacters and characteristics in literature
dc.subjectWahusika na sifa zao katika fasihi
dc.subjectMajuto katika fasihi
dc.subjectFamily abandonment in literature
dc.subjectKutelekeza familia katika fasihi
dc.subjectMahusiano ya nje ya ndoa katika fasihi
dc.subjectTabia za kingono katika fasihi
dc.subjectMaambukizi ya VVU katika fasihi
dc.subjectSwahili literature—History and criticism
dc.subjectProverbs in literature
dc.subjectMethali katika fasihi
dc.subjectRealism in literature
dc.titleMajuto ni mjukuu: Uchunguzi wa mhusika Ngoma katika riwaya ya ua la faraja
dc.typeArticle

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
Fuluge Adria (2024).pdf
Size:
255.54 KB
Format:
Adobe Portable Document Format

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed to upon submission
Description:

Collections