Usawiri wa eskatolojia ya Waafrika katika mbolezi za Wangoni

dc.contributor.authorDuwe, Martina
dc.date.accessioned2024-10-15T06:03:08Z
dc.date.available2024-10-15T06:03:08Z
dc.date.issued2020
dc.descriptionMakala iliowasilishwa na kuchapishwa kwenye Jarida la CHALUFAKITA mwaka 2020, Juz. No. 2
dc.description.abstractEskatolojia ni kipengele kimojawapo kinachodhihirisha falsafa ya jamii za Waafrika kulingana na mila na desturi zao. Tafiti nyingi zilizofanywa kuhusu dhana hii zimejiegemeza katika muktadha wa kiteolojia. Baadhi ya tafiti hizo ni zile zilizofanywa na Baloyi (2008) na Lup (2013). Licha ya kuwapo kwa tafiti hizo, dhana ya eskatolojia ya Waafrika hususani fasihi simulizi za jamii ya Wangoni bado haijamakinikiwa ipasavyo. Aidha, ni wazi kwamba fasihi simulizi ni fasihi inayobeba na kuibua maarifa ya kifalsafa yanayoisawiri jamii husika kulingana na kaida zao. Kwa mantiki hiyo, makala hii inajadili usawiri wa eskatolojia ya Waafrika katika kipera cha mbolezi hususani za jamii ya Wangoni ili kubainisha maarifa yanayobebwa katika kipera hicho. Makala hii ni matokeo ya utafiti uliofanyika kwa kutumia mbinu ya ushuhudiaji shirikishi katika matukio yanayoambatana na suala la kifo na mahojiano ya ana kwa ana na baadhi ya Wangoni katika mazingira yao halisi. Data zimechanganuliwa kwa njia ya maelezo. Data hizo zinaonesha kuwapo kwa eskatolojia ya Waafrika katika mbolezi za jamii hiyo. Hata hivyo, makala hii inajadili vipengele muhimu vitatu tu ambavyo ni: kuamini katika uwepo wa Mungu, mwendelezo wa maisha baada ya kifo na nguvu za waliokufa (mizimu).
dc.description.sponsorshipNil
dc.identifier.citationAPA
dc.identifier.issneISSN: 2591-7013
dc.identifier.issnprint ISSN: 2665-0789
dc.identifier.urihttps://scholar.mzumbe.ac.tz/handle/123456789/1448
dc.publisherCHALUFAKITA 2020, JUZ. NA. 2
dc.subjectEskatologia
dc.subjectWangoni
dc.subjectUsawiri wa Eskatologia
dc.subjectMbolezi
dc.subjectMizimu ya Wangoni
dc.subjectTanzania
dc.titleUsawiri wa eskatolojia ya Waafrika katika mbolezi za Wangoni
dc.typeArticle
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
Duwe, M.-(FSS)-(2020).pdf
Size:
332.77 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed to upon submission
Description:
Collections