Mitazamo ya Waafrika kuhusu urithishwaji wa mali: Uchunguzi wa bunilizi za Kiswahili

dc.contributor.authorDuwe Martina
dc.contributor.authorFuluge Adria
dc.date.accessioned2026-05-12T07:43:09Z
dc.date.issued2024
dc.description.abstractKurithisha mali katika jamii nyingi za Kiafrika ni suala linalohifadhi na kuendeleza utamaduni wa jamii. Hivyo, thamani ya mwanadamu katika ulimwengu wake hubainika pia kupitia mali anazorithisha wengine. Vilevile, kupitia mali hizo, mrithishaji anaendelea kuishi katika fikra za wanaorithishwa hata baada ya kifo chake. Kwa msingi huo, urithishwaji wa mali ni hazina inayoendeleza kizazi na kuleta kumbukumbu idumuyo katika ulimwengu halisi wa mwanadamu. Fasihi ni akiso la maisha ya mwanadamu katika mazingira yake halisi. Kwa mantiki hiyo, bunilizi za Kiswahili huhifadhi na kudokeza misingi mbalimbali inayozingatiwa katika kuendesha maisha ya jamii. Mathalani, ile inayohusu suala la urithishwaji wa mali kupitia wahusika wanaosukwa kwa ustadi unaokidhi haja ya kufikisha maudhui lengwa. Hata hivyo, haijaelezwa bayana mitazamo ya Waafrika kuhusu suala la urithishwaji wa mali kwa kuhusianisha na bunilizi za Kiswahili. Hivyo basi, makala hii imeshughulikia jambo hilo kwa kujiegemeza katika riwaya za Rosa Mistika (1971) na Dunia Uwanja wa Fujo (1975). Makala hii ni matokeo ya data zilizopatikana maktabani kwa kutumia mbinu ya usomaji. Vilevile, katika uchunguzi, uchanganuzi na uwasilishaji wa matokeo hayo, misingi ya Nadharia ya Sosholojia ya Kifasihi imetumika. Matokeo yanaonesha kuwa katika suala la urithishwaji wa mali kwa Waafrika, kuna mitazamo mbalimbali inayozingatiwa. Makala hii inajadili mitazamo mikuu mitatu, ambayo ni: mtazamo wa kitamaduni, kihiari, na kimabavu.
dc.description.sponsorshipPrivate
dc.identifier.citationAPA
dc.identifier.issn2412-6993
dc.identifier.urihttps://scholar.mzumbe.ac.tz/handle/123456789/1991
dc.language.isoother
dc.publisherMwanga wa Lugha
dc.subjectInheritance and succession — Africa
dc.subjectDecedents' estates — Africa
dc.subjectMali za marehemu
dc.subjectCustomary law — Africa
dc.subjectSheria za kimila
dc.subjectWills — Africa
dc.subjectWosia
dc.subjectRight of property — Africa
dc.subjectHaki ya umiliki wa mali
dc.subjectInheritance and succession — Social aspects
dc.subjectMitazamo ya kijamii kuhusu urithi
dc.subjectInheritance and succession — Religious aspects
dc.subjectMitazamo ya kidini - Uislamu
dc.subjectUkristo
dc.subjectInheritance and succession — Women
dc.subjectHaki za wanawake katika urithi
dc.subjectAfrican ethics
dc.subjectMaadili ya Kiafrika yanayohusiana na ugawaji wa mali
dc.subjectBunilizi
dc.subjectUrithi na Mali
dc.subjectUrithishwaji Mali
dc.titleMitazamo ya Waafrika kuhusu urithishwaji wa mali: Uchunguzi wa bunilizi za Kiswahili
dc.typeArticle

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Thumbnail Image
Name:
Duwe, M and Fuluge, A.- (2024).pdf
Size:
477.3 KB
Format:
Adobe Portable Document Format

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed to upon submission
Description:

Collections