Fuluge, Adria2026-08-282024APAhttps://doi.org/10.58721/jkal.v2i2.863https://scholar.mzumbe.ac.tz/handle/123456789/2204Paper submitted for publication in the Journal of Linguistics, Literary and Communication StudiesMaisha ya mtu ni hadithi inayopaswa kusimuliwa ili kutoa mafunzo kwa jamii kuhusu mapito ya mhusika. Hii inatokana na ukweli kwamba kila mtu katika jamii ana mambo mazuri na/au mabaya ya kusimulia yanayohusu mapito ya maisha yake. Yapo masimulizi yanayofurahisha kutokana na matendo ya mhusika na mengine husikitisha kiasi cha kumfanya mhusika kuyajutia maisha yake kutokana na kufanya au kutofanya jambo fulani. Kwa msingi huo, makala hii ililenga kuchunguza methali inayosema “majuto ni mjukuu” kwa kuchunguza maisha ya mhusika Ngoma katika riwaya ya Ua la Faraja (2004). Mhusika huyu ameteuliwa kama kiwakilishi cha wahusika wengi ambao katika maisha yao, walifanya na/au hawakufanya mambo fulani ambapo kutokana na kufanya na/au kutokufanya kwao, kulisababisha majuto katika maisha yao. Pia, riwaya hii imeteuliwa kama sampuli ya riwaya mbalimbali zenye wahusika wenye sifa kama za mhusika Ngoma. Data zilitokana na uchambuzi wa riwaya ya Ua la Faraja. Vilevile, Nadharia ya Uhalisia ilitumika kama mwongozo katika ukusanyaji wa data, uchambuzi na uwasilishaji wa matokeo ya utafiti wa makala hii. Matokeo yanaonesha kwamba ziko sababu kuu nne zilizosababisha Ngoma ayajutie maisha yake. Sababu hizo ni kukosa uaminifu katika ndoa, kuitelekeza familia yake, kuendekeza anasa, na kutowajali ndugu zake.otherMajutoMethaliMhusikaMjukuuCharacters and characteristics in literatureWahusika na sifa zao katika fasihiMajuto katika fasihiFamily abandonment in literatureKutelekeza familia katika fasihiMahusiano ya nje ya ndoa katika fasihiTabia za kingono katika fasihiMaambukizi ya VVU katika fasihiSwahili literature—History and criticismProverbs in literatureMethali katika fasihiRealism in literatureMajuto ni mjukuu: Uchunguzi wa mhusika Ngoma katika riwaya ya ua la farajaArticle