Languages and Communication Studies
Permanent URI for this community
Browse
Browsing Languages and Communication Studies by Subject "Falsafa"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Hatima ya maisha ya Waafrika katika Bunilizi za Kiswahili: Mwegamo wa kifalsafa(Ruaha Journal of Arts and Social Sciences (RUJASS), 2021) Duwe, MartinaMakala hii imefafanua sababu za hatima ya maisha ya mwanadamu kulingana na fikra za Waafrika kwa kurejelea riwaya za Utengano (1980) na Tata za Asumini (1990). Data za msingi zilizofafanuliwa katika makala hii zimepatikana maktabani kwa kutumia mbinu ya usomaji makini. Nadharia ya Udhanaishi imetumika kama mwegamo muhimu katika uchambuzi na mjadala wa data zilizowasilishwa katika katika utafiti uliofanyika. Matokeo yanaonesha kuwa utajiri wa maarifa yaliyomo ndani riwaya teule husawiri maudhui na fikra halisi za Waafrika kulingana na tamaduni zao. Fikra hizo hudhihirisha falsafa inayotawala maisha yao. Pia, hubainisha sababu mbalimbali za hatima ya mwanadamu kulingana na mitazamo ya Waafrika. Kifo ni miongoni mwa sababu zilizobainika wazi katika riwaya teule kuwa kinasababishwa na maamuzi ya Mungu, maovu ya mwanadamu mwenyewe na watu wanaomzunguka katika mazingira yake halisi; na namna Waafrika wanavyofikiri juu ya sababu za hatima ya maisha yao. Mwandishi anayaonesha haya ili kudhihirisha uhalisi wa fikra za jamii yake kama sampuli ya jamii za Kiafrika. Makala hii inahitimisha kuwa fasihi andishi inahifadhi na kuonesha maarifa yanayoisawiri jamii husika.